Maafisa elimu wa Kata 21 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma wametakiwa kuwa wabunifu na wachapakazi katika sehemu zao za kazi ili kuhakikisha wanafunzi wanaondokana na tatizo la kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu na hatimaye ufaulu wa wanafunzi katika shule zilizopo katika Halmashauri hiyo kuongezeka.
Hayo yamesemwa leo Jumatano 26, Septemba 2018 na Kaimu Afisa elimu Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. Sabato Arika wakati wa kikao kati yake na Maafisa elimu wa Kata 21 zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa kikao hiko Ndg. Arika aliwataka maafisa elimu hao kufahamu malengo ya Halmashauri na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ina mkakati wa kuhakikisha mwaka ujao wa masomo tunaondokana na tatizo la wanafunzi la kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) na hatimaye kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao katika shule zetu”* alisema Arika.
Jambo hili linawezekana kwa asilimia mia, kwa hiyo Maafisa elimu Kata mnatakiwa kuwa wabunifu na wachapakazi kuhakikisha malengo haya ya Halmashauri yanatimia na kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli”* alisema Arika.
Sambamba na hilo Kaimu Afisa elimu Wilaya ya Musoma Ndg. Sabato Arika, aliwataka Maafisa elimu hao kuhakikisha swala la utoro wa walimu katika shule zilizopo katika Kata zao linatokomezwa.
Pia kuna tatizo kubwa la utoro wa walimu, wengi hawaingii kwenye vipindi wanakuwa kwenye biashara zao binafsi, naomba swala hili mlifatilie na muhakikishe walimu wanakuwa katika maeneo yao ya kazi muda wote” alisema Arika.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa