Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imeshiriki kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha Mbwa Duniani ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mh. Anna Rose Nyamubi.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Ijumaa 28, Septemba 2018 katika kiwanja cha Mwenge Butiama kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.
Maadhimisho hayo yalijumuisha Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama na Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.
Maadhimisho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu ya Linda afya yako na ya wanyama wako kwa chanjo ya kila mwaka ya mbwa na paka hufanyika tarehe 28, Septemba ya kila mwaka.
Sambamba na hilo pia kulifanyika uzinduzi wa utoaji chanzo ya kichaa cha mbwa ambapo wafugaji walipata fursa ya kupata huduma ya kupata chanjo ya bure kwa mbwa wao.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa