Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma wamepokea mrejesho na mapendekezo sambamba na kutoa maoni juu ya kilichobainiwa na timu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii, SAM ( Social Accountability Monitoring).
Wakuu hao wa Idara na Vitengo wamepokea mrejesho huo kutoka kwa timu ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamiii (SAM) leo Jumatatu 24, Septemba 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo eneo la Uwanja wa ndege, Musoma.
Hatua hiyo ya kupokea mrejesho na mapendekezo sambamba na wakuu hao wa idara na vitengo kutoa maoni yao imekuja baada ya timu ya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii (SAM), kufanya kazi ya kupitia miradi mitatu ambayo ni mradi wa shamba la mbegu za mihogo unaosimamiwa na kikundi cha KEUMA, eneo la Maneke Kata ya Busambara, mradi wa pampu ya umwagiliaji unaosimamiwa na kikundi cha Tuvumiliane kilichopo eneo la Kigera Etuma Kata ya Nyakatende na mradi wa pampu ya umwagiliaji unaosimamiwa na kikundi cha Mapambano kilichopo eneo la Kwibara Kata ya Mugango tangu Mwezi Julai 2018.
Timu hiyo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii (SAM) iliyoundwa na wawakilishi wanne (4) kutoka AZAK, wakulima wawili (2), wataalamu watatu (3) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Madiwani wawili (2) ilipewa mafunzo maalumu juu ya ufuatiliaji wa miradi ya kilimo na wawezeshaji kutoka ANSAF na kuratibiwa na SHIMAKIUMU.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa