Wananchi wanaoishi Kata ya Mugango wamejitokeza kwa wingi katika kujitolea nguvu kazi ili kuweza kusaidia katika kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha Afya Mugango.
Wananchi hao kutoka vijiji vitatu vilivyopo Katika Kata hiyo ambavyo ni Kurwaki, Kwibara na Nyang’oma wameleta mchanga takribani roli ishirini (20) katika eneo lililotengwa kujenga majengo hayo.
Licha ya wananchi hao mpaka sasa kuleta mchanga huo (roli ishirini) bado wanaendelea na zoezi hilo.
Majengo yanayotarajiwa kujengwa katika Kituo hicho cha Afya ni jengo la kuhifadhia maiti, jengo la wodi ya kinamama, jengo la upasuaji, jengo la Maabara na nyumba ya mtumishi.
Wakati huo huo mifuko ya simenti elfu moja mia tatu na ishirini (1320) imewasili katika eneo hilo na hatua ya ufyatuaji wa matofali inaendelea.
Pia msingi kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo matano (kwa kila jengo) unaendelea kuchimbwa na mafundi (local fundi) wanaojenga majengo hayo.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa