Mradi huu wa ujenzi wa jiko la gesi ni sehemu ya juhudi za kampuni ya MMG Gold Limited kupitia mpango wa Corporate Social Responsibility (CSR) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma katika kusaidia jamii kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia — jambo linaloendana moja kwa moja na Ajenda ya Dunia kuhusu Nishati Safi na Uhifadhi wa Mazingira.
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 26,805,102/=
Majiko ya kupikia ikiwa ni matumizi ya nishati safi ya kupikia jambo linaloendana moja kwa moja na Ajenda ya Dunia kuhusu Nishati Safi na Uhifadhi wa Mazingira.
Kupitia mradi huu, shule itapunguza matumizi ya kuni na mkaa, hivyo kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuboresha afya ya wapishi na wanafunzi wanaohudumia chakula.

Tunawashukuru MMG Gold Limited, uongozi wa shule, na wadau wote walioshiriki kufanikisha utekelezaji wa mradi huu muhimu.
Kiwanda cha Kufyatua Tofali (Makao Makuu – HQ)
Mradi wa MUSEKELA COMPANY LTD unahusisha kiwanda cha kufyatua tofali kilichopo katika Makao Makuu (HQ).

Kwa sasa, matengenezo ya mashine yamekamilika kikamilifu na kiwanda kipo tayari kuanza shughuli za uzalishaji wa tofali.
Mradi wa SWASH (School Water, Sanitation and Hygiene) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 unatekelezwa katika Shule ya Msingi Nyabaengere kwa lengo la kuboresha miundombinu ya maji safi, usafi na afya shuleni.
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 48,649,442.83/=
Hatua iliyofikiwa, Ujenzi wa matundu 17 ya vyoo umekamilika kwa kiwango kikubwa.

Kazi zilizobaki ni kufunga vigae katika korido, kufunga mifereji ya maji (gata), na kukamilisha awamu ya pili ya mifumo ya maji ili vyoo viweze kuanza kutumika rasmi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa