Kwa kawaida Halmashauri ya Wilaya ya Musoma hupata mvua mara mbili kwa mwaka (Bimodal). Mvua hizo ni za masika na vuli; Mvua za vuli ni za muda mfupi ambazo hunyesha kuanzia mwezi Oktoba - Desemba. Mvua za masika hunyesha kati ya mwezi Machi na Mei na baada ya hapo hufuatia kipindi cha kiangazi/ukame kati ya mwezi Juni na Oktoba.
Wastani wa mvua kwa mwaka ni 500mm hadi 700mm. Halmashauri ina jumla ya hekta 108,675 zinazofaa kwa kilimo, maeneo wanayolima ni yenye ukubwa kati ya 1/8 ya ekari hadi ekari 5. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kilimo hufanywa na wakulima wadogo wadogo ambapo mazao yanayolimwa ni Muhogo, Mtama Mahindi, viazi vitamu, Mpunga, Pamba, Dengu na Alizeti.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa