Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa Shule za Sekondari.
Kubuni Mipango ya Mitihani ya Elimu ya Sekondari na kusimamia utekelezaji wake
Kuhakikisha kuwa Walimu na watumishi wengine wa shule za Sekondari wanafanyiwa tathimini ya wazi ya utendaji kazi (Open Perfomance Review and Appraisal System – OPRAS)
Kukusanya, kuchanganua, kutuma na kutoa takwimu sahihi za elimu za Sekondari katika Halmashauri
Kubuni na kuratibu mipango ya mafunzo kazini kwa Walimu na watumishi wengine wa shule za Sekondari
Kuratibu mashindano ya michezo ya Taaluma ya shule za Sekondari katika Halmashauri
Kuratibu utoaji wa huduma mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri
Kuandaa malipo ya nauli kwa walimu wanaokwenda likizo
Kuandaa bajeti ya Idara na Vitengo vyake ikiwa ni pamoja na mpango kazi inaoendana na bajeti hiyo.
Kuandaa Tange ya walimu wa shule za Sekondari kwa kila mwaka