Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Masharti ya kupata leseni ya biashara
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria.
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
Utaratibu wa kupata leseni ya biashara
Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN 2110 kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:-
(i) Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of Incorporation or Registration).
(ii) “Memorandum and Article of Allocation” kama ni Kampuni
(iii) Kitambulisho cha mpiga kura, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).
(iv) Hati ya kiuwakili (prowess of a Honey) kama wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi.
(v) Ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara(Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali , Kwa mfano (TFDA,EWURA, TAURA, CRB, TILLI) n.k lazima mwomaji kuwa na leseni husika kablaya kuomba leseni ya biashara fomu ya maombi ya biashara (TFN211) hutolewa kwa ada ya Tshs. 1,000/=.Baada ya kujaza fomu na viambatanisho, maombi hupitishwa ngazizinazotakiwa kisheria – Mpango Miji na Afya. Baada ya hapo leseni hutolewa ndani ya siku moja au mbili na si zaidi.Angalizo: Kwa utaratibu wa kuanzia mwaka 2004/2005 leseni mpya hutolewa bila malipo ya ada za leseni na leseni zote hutolewa mara moja tu hadi sheria mapya (BARA) itakapoanza kutumika.
Masharti ya utumiaji wa leseni
1. Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi.
2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.
3. Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya Biashara No. 25 ya 1972.
4. Mwenye leseni hatapewa huduma/bidhaa amao hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na vyombo vinavyotumika kisheria.
5. Mwenye leseni anaweza kunyaganywa wakati wowote ikiwa itaonekana aliipata kwa njia ya danganyifu au amekiuka msharti ya leseni.
Makosa
i. Kuendesha biashara bila leseni.
ii. Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye leseni.
iii. Kutumia leseni moja kufanyia biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi.
iv. Kushindwa kuonyesha lesenid ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyeidhinishwa na Serikali.
v. Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi.
vi. Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada/kodi inayostahili.
vii. Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.
Adhabu
Mtu yeyote anayetenda majawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tshs. 50,000/= na isiyozidi Tshs. 100,000 au kifungo kisichozidi miaka miwili (2) au faini na kifungo kwa pamoja.
Leseni za vileo
Sheria ya leseni za vileo imenyambulisha aina tisa za leseni za vileo zinazoweza kutolewa chini ya sheria hii: Retailers On Leseni hii humruhusu mwenye biashara kuuza pombe na kunywa eneo la biashara.
Retailers off
Leseni hii haimruhusu mtu kinywea pombe eneo la biashara bali kwa watuwanaochukua kunyewea majumbani (Take away) kama Groceries.
Wholesale
Leseni hii ni kuuza pombe kwa jumla
Hotel
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa ajili ya kunywea katika eneo la biashara kwa watu waliopanga hotelini kwa wakati wowote wa mchana na usiku.
Restaurant
Leseni hii inamruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa mtu yeyote anayekula chakula katika mgahawa katika muda wa saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 hadi saa 6.00 usiku.
Members club
Leseni hii huruhusu uuzaji wa pombe kwa kiasi chochote kwa mwanachama wa Klabu na wageni wao tu.
Combined
Leseni ambazo zimeambatanishwa mhili kwa pamoja:
(a) Combined Hotel and retailers on
(b) Combined Hotel and Restaurant
(c) Combined restaurant and retailers on
Temporary
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni mahali penye burudani, starehe au mkusanyiko mwingine kwa kipindi kisichozidi siku tatu.
Local liquor
Class a local liquor
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kutengeneza pombe za kienyejikatika sehemu iliyotajwa na kuuza kwa ajili ya kunywea sehemu yabiashara au nje ya sehemu ya biashara.
Class B Local Liquor
Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji sehemu iliyotajwa na kwenda kuuzia sehemu nyingine iliyo na leseni ya kuuza pombe za kienyeji
Class C Local Liquor
Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni na kuuza kwa mwenye class D au Class E
Class D Local Liquor
Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni kwa kunywea eneo la biashara.
Class E Local Liquor
Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji kwa ajili ya kunyewea sehemu nyingine mbali ya eneo la biashara
1. Masharti ya kupata leseni
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya Vileo ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria.Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
2. Utaratibu wa kupata leseni
Mwombaji hujaza fomu za maombi zinazotolewa na Manispaa
Eneo/jingo linalokusudiwa kufanyia biashara hiyo kukaguliwa na Afisa Afya, Afisa Mipangomiji, Polisi, Afisa Mtendaji wa Kata (WDC) na Afisa Biashara wa Manispaa na hutoa maoni yao kwenye fomu husika.
Maombi hayo hupelekwa katika Malaka ya Utoaji wa Leseni za Vileo ya Halmashauri kwa uamuzi
Mwombaji ambaye maombi yake yamepitishwa hupewa Leseni baada ya kulipa ada inayotakiwa na ni lazima amekamilisha masharti ya kupata leseni hapo juu
3. Masharti ya utumiaji
Leseni za vileo zina masharti mengi ikiwa ni pamoja na kutouza kilevi kwa watoto. Masharti mengine ni muda wa kuuza pombe na kelele za muziki.
Makosa
Baadhi ya makosa chini ya sheria hii:
Kuruhusu biashara nyingine isiyokubalika kisheria kufanyika eneo la biashara
Kuuza pombe kwa mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita(16)
Kuajiri mtu chini ya miaka kumi na sita (16) kuuza pombe
Kuruhusu mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita kukaa eneo la kuuzia pombe
Kutoweka leseni sehemu ya wazi, ambapo itaonekana kwa urahisi na wakaguzi
Kumruhusu/kuleta fujo katika eneo la biashara
Kuruhusu eneo la biashara kutumika kama danguro
Kuuza pombe muda ambao ni kinyume cha sheria
Kufanya biashara ya pombe kwa kutumia leseni ya vileo ambao haistahili
Adhabu
Mfanyabiashara anayetenda mojawapo ya makosa haya akikamatwa,atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atalipa faini au kifungo au adhabu zote kwa pamoja.
II Utaratibu wa ushuru wa malazi (hotel levy) chini ya sheria na.23 ya 1972
IMETOLEWA NA AFISA BIASHARA
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa