Majukumu ya Idara ni kutoa michango ya kimkakati kwa menejimenti katika mambo yahusuyo Utawala na menejimenti ya rasilimali watu kama ajira, uendelezaji rasilimaliwatu, uelimishaji, upandishaji vyeo, menejimenti ya utendajikazi na kushughulikia maslahi ya watumishi.
Idara inatunza na kuhuisha kumbukumbu za rasilimali watu na kutoahuduma za kiutawala ili kuhakikisha mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Kuhakikisha kuwa utumishi wa umma unaendeshwa kwa kuzingatia sera,sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali katika utumishi wa umma.
Kufuatilia na kutafsiri sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma na kusimamia uwianishaji wa ajira katika utumishi wa umma ndani ya Halmashauri kwa kufuata kanuni na taratibu zote zilizowekwa na Serikali.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa