Leo Jumanne tarehe 16 Desemba, 2025, kumefanyika Kikao cha Kamati ya Ufuatiliaji na Tathmini ngazi ya Taasisi (CMT) katika Ukumbi wa Mkurugenzi Mtendaji, kikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela Nitu Palela.
Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa mipango na shughuli za taasisi, kufanya tathmini ya maendeleo yaliyofikiwa, pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji na ufanisi katika kipindi kijacho. Wajumbe wa kamati walipata fursa ya kuwasilisha changamoto zilizopo na kupendekeza hatua stahiki za kuzitatua.
Aidha, kikao kilisisitiza umuhimu wa ufuatiliaji endelevu, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali ili kuhakikisha malengo ya taasisi yanafikiwa kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika.
Kamati iliahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na menejimenti ili kuhakikisha maazimio yote yaliyopitishwa yanatekelezwa ipasavyo kwa manufaa ya taasisi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa