Wakulima wadogo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma katika Mkoa wa Mara wapatiwa vifaa vya umwagiliaji na kuishukuru Serikali kufuatia kutokana na matarajio ya kuongeza uzalishaji na kipato kupitia kilimo cha umwagiliaji.
Akizindua matumizi ya vifaa hivyo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), amesema Serikali ya Awamu ya Sita ina matumaini makubwa na kilimo cha umwagiliaji katika kuwawezesha wakulima wadogo kulima kwa uhakika.
Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Agenda 10/30 yenye kulenga kukuza kilimo kwa asilimia ifikapo mwaka 2030, akisisitiza kuwa matumizi ya teknolojia za kisasa za kilimo yamekuwa nguzo muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Kwa upande wake, Mratibu wa Programu ya TFSRP, Bw. Timothy Semuguruka, amesema Mkoa wa Mara umenufaika na mpango huo baada ya tathmini kubaini uwepo wa vyanzo vya kudumu vya maji. “Vifaa hivi vitawawezesha wakulima kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza tija na kutumia ardhi yao kikamilifu kwa kilimo cha umwagiliaji,” amesema Semunguruka.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Juma Chikoka ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kupeleka vifaa hivyo wilayani humo, akibainisha kuwa uwekezaji huo unakwenda kuchochea maendeleo ya kilimo kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya bustani na kuimarisha uchumi wa wananchi wa Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa