Kaimu Afisa Michezo, Utamaduni na Sanaa wa Halmashauri ya Wilaya Musoma Bi. Rosalia Magoti Leo Februari 3, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri amewaeleza Walimu wa michezo wa Shule za Msingi na Sekondari kuwa hawatakubali kushindwa tena katika michezo hivyo wazingatie Miongozo ya mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa kuzingatia Umri wa wanafunzi wanaotakiwa kushiriki mashindano waliosajiriwa kwenye mfumo pamoja na Kufundisha michezo yote iliyopo kwenye miongozo ambayo inatakiwa kuwepo kwenye mashindano.
Amesisitiza pia kuwa Viwanja vyote viwe na vipimo sahihi pamoja na uwepo wa vifaa vya Michezo mashuleni
"Wafuatilieni wanafunzi wote walioshiriki mashindano ngazi ya Taifa mwaka jana 2023 ili waendelee kushiriki michezo hiyo" Amesisitiza Bi. Rosalia
Aidha Walimu wa riadha wameomba vigezo vya riadha viletwe mapema ili waweze kuandaa timu kwa kuzingatia vigezo. Pia Walimu wa Basketball wameomba Uwanja uliopo Kasoma Sekondari ukarabatiwe ili mchezo huu ushiriki katika mashindano kwa mwaka 2024 sambamba na Table Tenis.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa