Madiwani 28 wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, wakiwemo madiwani 21 wa kata na madiwani 7 wa viti maalumu, wamekula kiapo leo tarehe 05 Desemba 2025 mbele ya Hakimu. Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni hatua muhimu ya kuwawezesha kuanza rasmi majukumu yao ya kuwatumikia wananchi katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.
Madiwani hao wamechaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, na wanatarajiwa kushirikiana kwa karibu na watendaji wa Serikali katika kupanga, kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Aidha, uongozi wa Halmashauri umeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha madiwani wanatimiza wajibu wao kwa ufanisi, huku wakisisitiza umuhimu wa uadilifu, uwajibikaji na ushirikiano katika kuleta maendeleo endelevu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa