Leo Septemba 13, 2023 katika Kituo cha Afya Murangi, Afisa Muuguzi Bi.Sophia Kassim kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando amewapa mafunzo watumishi wa kituo hiki cha Murangi namna ya kushughulika na mtoto mchanga ambaye hakuweza kulia au kupumua baada ya kuzaliwa. Amewasisitiza kuwa mara baada ya mtoto kuzaliwa anatakiwa kukaushwa vizuri ili kupata joto na kuangalia njia ya hewa kuona kama iko sawa.
Ameshauri uwepo wa vifaa vya kumsaidia mtoto kabla ya kuzaliwa ili kutoa huduma kwa wakati pindi changamoto yoyote itakapojitokeza.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa