Mkurugenzi Mtendaji (W) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma amefunga mafunzo maalumu yaliyofanyika tarehe 26 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Jengo la Utawala – Afya, Kwikonero, yakilenga kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Vijiji kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.
Mafunzo haya yamelenga kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa afua za lishe katika ngazi ya kijiji, na hivyo kuchochea ustawi wa afya ya jamii hususan watoto na mama wajawazito.
Mada zilizowasilishwa ni pamoja na:
* Dhana ya lishe, makundi ya vyakula na umuhimu wake
* Sheria ndogo za lishe
* Mwongozo wa Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALiKi)
* Zana ya upimaji na tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe
* Mwongozo wa uchangiaji wa chakula shuleni (kiasi kinachohitajika kwa kila mwanafunzi na wajibu wa kijiji)
* Hamasa za lishe kupitia vikundi vya lishe, klabu, sanaa na mabango ya afya
Kupitia mafunzo haya, washiriki walikubaliana kutekeleza maazimio yafuatayo:
1. Kila kijiji kuanzisha daftari maalumu lenye orodha ya watoto wote walio chini ya miaka mitano.
2. Kila kijiji kuhakikisha maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALiKi) yanafanyika kwa ufanisi.
3. Kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu utoaji na uchangiaji wa chakula shuleni.
4. Kuhakikisha mafunzo na ujenzi wa uwezo kwa watekelezaji wa mkataba wa lishe, ikiwemo wenyeviti wa vijiji, yanaendelea kwa utaratibu endelevu.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji (W) amewaagiza viongozi hao kuanza mara moja kutoa hamasa juu ya kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe** itakayofanyika kuanzia 1 – 31 Desemba 2025.
Lengo kuu ni kuhakikisha kila mlengwa anapatiwa matone ya vitamini A pamoja na huduma nyingine muhimu za lishe.
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma inaendelea kuimarisha juhudi za kuboresha afya na lishe ya wananchi wake kupitia ushirikiano na viongozi wa vijiji, wataalam, wadau na jamii kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa