Maadhimisho ya kilele cha Mara Day yamefanyika kwa mafanikio katika Uwanja wa Mwenge, Butiama, tarehe 15 Septemba 2025. Maadhimisho haya yamekusanya wadau mbalimbali wa mazingira, viongozi wa serikali, na wananchi kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Mara.
Mgeni rasmi katika maadhimisho haya alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Kanali Evans Alfred Mtambi, ambaye alisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kulinda mazingira.
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Kanali Mtambi alikabidhi cheti cha kutambua mchango (Certificate of Appreciation) kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela Nitu Palela, kutokana na mchango wake mkubwa katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uhifadhi wa mazingira katika halmashauri hiyo.
Maadhimisho yalipambwa na burudani mbalimbali za kitamaduni, maonesho ya kazi za jamii na taasisi, pamoja na ujumbe wa kuhamasisha utunzaji wa rasilimali za asili kwa maendeleo endelevu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa