Leo, Disemba 10, 2025 — Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Juma Chikoka, ameongoza kikao cha kawaida cha Ushauri cha Wilaya (DCC) kilichofanyika leo kwa lengo la kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na masuala ya utawala na ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Musoma.
Kikao hicho kimehusisha wadau na viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Musoma. Miongoni mwa washiriki wakuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela N. Palela, pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Ndugu Bosco O. Ndunguru, ambao kwa pamoja waliwasilisha taarifa juu ya utekelezaji wa majukumu ya halmashauri hizo mbili.
Aidha, kikao kimehudhuriwa na wawakilishi mbalimbali kutoka ndani ya Wilaya ya Musoma wakiwemo:
* TARURA – kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya barabara;
* TANESCO – kwa ajili ya masuala ya nishati na upatikanaji wa umeme;
* MUWASA – wakizungumzia hali ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama;
* Mradi wa Maji wa Mugango–Kiabakari;
* Viongozi wa Vyama vya Siasa;
* Viongozi wa Dini, wakichangia maoni juu ya ustawi wa jamii.
Katika kikao hicho, washiriki wamejadili mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha robo mwaka, changamoto zinazoikabili wilaya pamoja na mikakati ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi. Mhe. Chikoka amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya taasisi zote na kuwataka viongozi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.
Kikao kimehitimishwa kwa kuweka maazimio na kutoa maelekezo ya utekelezaji katika maeneo ya kipaumbele, ikiwemo miundombinu, afya, elimu, maji na nishari.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa