Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka Leo Novemba 11, 2025 katika kikao Cha tathmini ya mkataba wa lishe Kwa robo ya kwanza 2025/2026, ameipongeza Kata ya Makojo Kwa ushiriki bora wa SALiKi na kutumia jukwaa hilo Kwa shughuli jumuishi
Wajumbe wa kikao hicho ambao ni Wakuu wa Idara mtambuka zinazotekeleza mkataba wa lishe(Elimu, Mipango, Kilimo, na Fedha),maafisa lishe na watendaji wa Kata wameipongeza pia Kata ya Makojo na kuahidi kuiga mfano katika utekelezaji wa SALiKi katika maeneo yao.
Lengo la SALiKi katika maeneo yetu ni kuifahamisha jamii kuwa msingi wa afya zetu kwa ajili ya kuendeleza uhai, hali njema ya afya na nguvu kazi yenye tija katika jamii unatokana na chakula unachokula.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa