Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. Said Mtanda amewataka Maafisa habari ngazi za Halmashauri pamoja na Mkoa kuwa wabunifu na kutojigeuza kuwa waandishi wa habari Bali watimize majukumu yao. Kauli hiyo ametoa kwenye kikao walichokutana na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mara Leo Desemba 29 ,2023 katika ukumbi wa uwekezaji kilichowashirikisha maafisa habari kutoka kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Mara. Mtanda alisema Waandishi ni chachu ya kusukuma maendeleo kwa jamii hivyo hawana budi kushirikishwa Kwa kupewa taarifa na kuwa huru katika kutekeleza majukumu yao ya kazi. Aidha amewataka Maafisa habari hao na viongozi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano Kwa waandishi wa habari Kwa kuwapa taarifa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao . "Ukiona umeandikwa una mapungufu usichukie mwaandishi wa habari alindwe na apewe uhuru wa kutekeleza majukumu yake "amesema Mtanda. Aidha Mtanda amewashukuru na kuwapongeza waandishi wa habari mkoani hapa Kwa kufanya kazi zao Kwa waledi Kwa kipindi alichofika mkoani hapo na kuwataka kuendelea na utendaji wao Kwa uhuru na endapo jambo litaenda tofauti wasisite kumjulisha. Licha ya hayo Mtanda alisema anao uzoefu Katika tasnia ya habari hivyo anafahamu umuhimu wao ambapo amewakumbusha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli , zisizoegemea upande mmoja na kuandika habari za uchunguzi na uibuaji. Nao Waandishi wa habari wememshukuru Mkuu wa Mkoa huyo kuthamini na kutambua umuhimu wa mchango wao na kwamba yeye ndie Mkuu wa Mkoa pekee alifungua ukurasa Mpya wa kukutana nao Kwa lengo la kutaka ushirikiano wa kufanya kazi Kwa pamoja Kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Mara. Lengo la kikao cha kukutana na waandishi wa habari ni kuangalia yaliyofanyika mwaka huu wa 2023 na changamoto na kuona namna ya kwenda mwaka mpya wa 2024.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa