Leo Mei 16 ,2024 katika ukumbi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Musoma , Kikao cha Lishe robo ya tatu kuelezea utekelezaji wa Afua za Lishe kimefanyika kikiazimia kutoa msisitizo kwa Shule zote za Msingi na Sekondari kuendeleza Elimu ya kujitegemea kwa wanafunzi kuzalisha mazao ambayo yatasaidia kupata chakula shuleni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. Msongela Palela amesema mbali na kuendeleza Elimu ya kujitegemea, Idara ya Kilimo itoe ushirikiano wa kutosha katika shule hizo kwa kutoa elimu na ushauri wa Kilimo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Idara zimeeleza jinsi shule zinavyotekeleza Afua za Lishe ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya matunda, kuanzisha bustani mashuleni pamoja na kuhimiza wazazi kuchangia chakula cha watoto wao.
Ndg. Palela amezitaka Idara zote kutekeleza bajeti zilizopangwa katika Idara hizo kwa wakati Ili kufikia malengo ya Mkataba wa Lishe Kwa Mwaka 2024/2024
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa