Timu ya Wataalam kutoka Divisheni na Vitengo mbalimbali imetekeleza ziara ya ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Ziara hii imelenga kutathmini hatua za utekelezaji wa miradi hiyo, kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana, na kubaini changamoto zozote zinazoweza kuathiri uhai na ubora wa miradi.
Katika ukaguzi huo, timu imepitia maeneo mbalimbali ambapo miradi inaendelea kutekelezwa, ikiwemo kukagua hatua za ununuzi, uchambuzi wa vielelezo vya manunuzi, ukaguzi wa vifaa vya ujenzi vilivyopo stooni, pamoja na uhakiki wa ubora wa kazi zilizokamilika na zile zinazoendelea. Aidha, wataalam wamefanya uhakiki wa matumizi ya malighafi, ukaguzi wa nyaraka za usimamizi wa mradi, na mazungumzo na wasimamizi wa miradi ili kupata taarifa za kina kuhusu maendeleo na changamoto zilizopo.
Timu imeendelea kusisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za manunuzi, usimamizi madhubuti wa miradi, na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa