Wakulima wadogo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma wamepata neema baada ya kukabidhiwa jozi za mashine za umwagiiaji. Vifaa hivyo vimetolewa kama sehemu ya juhudi za serikali kuboresha kilimo cha umwagiliaji na kuongeza uzalishaji wa mazao ya bustani na mbogamboga.
Katika juhudi za kuboresha kilimo na kuhakikisha usalama wa chakula nchini, Wizara ya Kilimo kupitia Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula (Tanzania Food Systems Resilience Program - TFSRP), imekabidhi vifaa vya kisasa vya umwagiliaji kwa vikundi vya wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na pampu za maji, mipira ya umwagiliaji, mabomba, na vinyunyizi vya umwagiliaji ambavyo vitasaidia kuongeza ufanisi katika kilimo cha umwagiliaji hasa wakati wa vipindi vya ukame.
Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika Halmashauri ya Wilayaya Musoma, yakihusisha kata 21 zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Mradi huo unalenga kuwawezesha wakulima wadogo kutumia teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji ili kuongeza tija, kupunguza utegemezi wa mvua, na kuhakikisha uzalishaji wa mazao kwa mwaka mzima.
Baadhi ya wakulima walionufaika na mpango huo wameishukuru serikali kwa kuwapatia msaada huo, wakisema utaleta mabadiliko makubwa katika maisha yao wakibainisha kuwa kwa muda mrefu wamekuwa
wakitegemea mvua katika kilimo, hali iliyokuwa ikisababisha changamoto wakati wa vipindi vya ukame.
Kupitia vifaa hivi vya umwagiliaji, sasa watakuwa na uhakika wa mavuno na soko la mazao yao kwa mwaka mzima. Ugawaji wa vifaa hivyo ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali za kuendeleza kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji, kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa na kilimo chenye tija, cha kibiashara, na chenye mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa