Jumatatu 05.02.2024
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said. Mtanda ameongoza kikao kazi Cha Timu za Menejimenti za Halmashauri zote tisa za Mkoa kujadili masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2024/2025.
Kikao kimeazimia Halmashauri zote kwa kipindi hiki Cha Maandalizi ya Mpango na Bajeti kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri hasa miradi ya Maendeleo yenye manufaa na matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi.
Katika eneo hili Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri kubuni na kuanzia miradi mizuri yenye tija itakayoongeza mapato katika Halmashauri na katika hilo Wataalamu wamekumbushwa kufanya upembuzi yakinifu wa Maeneo ya kuanzisha miradi hiyo yawe ni Maeneo yenye kuleta matokeo ya Uwekezaji.
Aidha Kikao kimeangazia pia makusanyo ya mapato kupitia mashine za PoS na kutoa angalizo wa upotevu wa mapato kupitia njia mbalimbali za udanganyifu kutoka kwa wakusanya mapato.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa