CSR kutoka MMG GOLD LIMITED – Ujenzi wa Jengo la Zahanati Mpya ya Seka (kuanzia msingi hadi hatua ya boma kukamilika)
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 50,000,000/=

Hatua iliyofikiwa.

Kazi za ujenzi wa jengo la zahanati mpya ya Seka zimefikia hatua nzuri ambapo boma limekamilika kikamilifu, hivyo hatua ya kwanza ya mradi imekamilika kwa asilimia 100%.

Kwa sasa, tunasubiri hatua ya pili ya utekelezaji ambayo itahusisha kazi za ukamilishaji wa jengo, ikiwemo upauaaji, umaliziaji wa ndani, mifumo ya maji na umeme ili jengo liweze kuanza kutumika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

Mradi huu umefadhiliwa kupitia mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) wa MMG Gold Limited, ukilenga kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo la Seka na vijiji jirani.
Tunawashukuru wadau wote waliounga mkono juhudi hizi za maendeleo.
Mradi wa BOOST unahusisha ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa na vyoo vyenye jumla ya matundu tisa (9) – wavulana (ME) 4 na wasichana (KE) 5.
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 119,923,697/=.

Hatua ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo hadi sasa.

Kwa sasa, ujenzi umefikia hatua ya msingi kwa vyumba vyote vinne na vyoo vyote tisa, sambamba na kazi ya kuweka hardcore (setting).
Mradi wa BOOST: Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo matundu sita vya wavulana katika Shule ya Msingi Bwasi B unaendelea vizuri
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 88,623,697/=.

Kwa sasa, ujenzi umefikia hatua ya kufunga lenta ya juu ya jengo la madarasa, huku kazi ya kunyoosha ukuta wa vyoo ikiendelea katika kozi ya tatu.
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 250,000,000/=.
Hatua iliyofikiwa;

Kazi za ujenzi zinaendelea vizuri ambapo boma la jengo la maabara na jengo la OPD (Out Patient Department) viko katika hatua nzuri ya ujenzi.

Aidha, ujenzi wa mashimo ya vyoo umeanza na unaendelea kufanyika kwa kasi.

Mradi huu unatekelezwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Kata ya Kataryo na maeneo jirani, kupitia upatikanaji wa miundombinu bora na ya kisasa ya afya.
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 31,000,000/=

Hatua iliyofikiwa

Ufungaji wa mbao za dali (brandering) umekamilika kwa madarasa yote mawili.

Ujenzi wa shimo la vyoo, boma, na upauaji umekamilika kwa mafanikio.

Mradi huu unatekelezwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa Shule Shikizi ya Karusenyi kwa kuongeza nafasi za madarasa na miundombinu bora ya vyoo.
Mradi huu unatekelezwa kupitia programu ya BOOST kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule kwa kujenga madarasa 5 na vyoo matundu 12 katika Shule ya Msingi Jitirora.
Jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni Tsh 158,723,697/=
Kazi za ujenzi zimefikia hatua nzuri kama ifuatavyo:

Madarasa 2 ya Awali na vyoo matundu 6
Ujenzi umefikia hatua ya renta
Vyoo vimefikia hatua ya kumwaga jamvi

Madarasa 3 ya Msingi
Mafundi wako eneo la kazi na hatua iliyofikiwa ni kupanga hardcore
Mradi huu unatekelezwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa Jitirora Primary School na kuongeza upatikanaji wa miundombinu rafiki kwa elimu bora.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa