Leo Ijumaa tarehe 19 Desemba, 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imefanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kuchagua eneo linalofaa kwa ajili ya ujenzi wa stendi.
Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela Palela, akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Katika ziara hiyo, Menejimenti imepata fursa ya kukagua na kutathmini maeneo yaliyopendekezwa, kuangalia miundombinu iliyopo, upatikanaji wa huduma muhimu pamoja na manufaa ya eneo husika kwa wananchi na maendeleo ya Halmashauri kwa ujumla.
Ziara hii ni sehemu ya jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma katika kuboresha huduma za usafiri na kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wake. Hatua zinazofuata zitahusisha tathmini ya kitaalamu na maamuzi ya mwisho kuhusu eneo litakalotumika kwa ujenzi wa stendi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa