Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Juma Chikoka, akiwa ameambatana na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, alifanya ziara ya mguu kwa mguu yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ziara hiyo ililenga kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kutumia fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na kukagua maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi watakaoanza masomo ya elimu ya awali na shule za msingi kwa mwaka wa masomo 2026.
Aidha, Mhe. Chikoka alisisitiza kuwa kabla ya tarehe **13 Januari, 2026, vyumba vyote vya madarasa vinavyotekelezwa vikamilike ili wanafunzi watakapofungua shule waweze kuanza masomo na kutumia vyumba hivyo bila changamoto.
Ziara hiyo imefanyika katika Shule ya Msingi Kasoma na Shule ya Msingi Suguti, ambapo alikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa na kutoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa