Wazazi na wanajamii wote kwa ujumla wajishangaa kwa kukumbushwa majukumu yao na huyu mtoto katika utangazaji wa simulizi za mafanikio katika kijiji cha Kwikuba Halmashauri ya Wilaya ya Musoma tarehe 25/05/2018
Waziri wa kilimo Eng. dkt. Charles John Tizeba akiwa katika ziara yake kijiji cha Kwibara Kata ya Mugango katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma tarehe 17/03/2018 ameagiza kuwa zao la pamba linunuliwe kwenye vyama vya ushirika tu na si vinginevyo.
Kwa wale wote ambao hawajajiunga na vyama hivi, sasa ndio wakati wa kujiunga kwani wasipofanya hivyo hawataweza kuuza zao hilo la pamba.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney akamata samaki waliochini ya ukubwa unaohitajika waliokuwa wanasafirishwa kwa uficho kutoka mwalo wa Bwai (Musoma vijijini) kuelekea Musoma Mjini. Akiongea na wananchi wa eneo la tukio leo tarehe 23/2/2018 katika kijiji cha Nyakatende, amekemea tabia mbaya ya baadhi ya wananchi kuendekeza biashara haramu hii ya uvuvi haramu
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa