• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Musoma District Council
Musoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maji
      • Ujenzi
      • AFYA
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • AFYA
    • KILIMO
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayoanzishwa
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Mikataba ya huduma kwa wateja
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi

Video

  • MWENGE WA UHURU 2024 WASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA NEST

    August 9th, 2024

    Mwenge wa Uhuru 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, wasisitiza matumizi ya Mfumo wa Nest katika manunuzi yote yanayofanyika katika Taasisi zetu

  • UUZAJI WA VIWANJA VYA MAKAO MAKUU

    December 7th, 2022

    Sasa unaweza kupata viwanja vilivyoko Makao makuu ya Halmashauri Mkabala na Hospitali ya Wilaya kwa bei nzuri sana.Wahi sasa kwa maana vimebaki vichache sana

  • KAYOMBO AKEMEA VITENDO VYA KISHIRIKINA BUGOJI

    October 13th, 2018

    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. John Lipesi Kayombo amewataka Diwani wa Kata ya Bugoji, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugoji, Wenyeviti wa kamati za msingi Kanderema ‘A’ na ‘B’ pamoja na wananchi kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja vitendo vya kishirikina vinavyoendelea katika shule hizo vinatokomezwa.


    Mkurugenzi Kayombo ametoa maagizo hayo Jana Ijumaa 12, Oktoba 2018 wakati wa kikao cha pamoja kati yake na viongozi wa Kata ya Bugoji, viongozi wa Kijiji cha Bugoji, walimu wa shule za Msingi za Kanderema ‘A’ na Kanderema ‘B’ pamoja na wananchi wa Kijijij cha Bugoji.


    Kikao hicho kimefanyika baada ya kuripotiwa matendo mengi ya kishirikina wanayokutana nayo walimu pamoja na wanafunzi wa shule hizo tangu mwaka 2013 mpaka sasa.


    Matendo hayo ya kishirikina yaliyoripotiwa yakiwemo ya wanafunzi kuanguka darasani, kupotea kimazingara kwa vitu mbalimbali vikiwemo simu, mboga, kihifadhi chaji (power bank),kufunguliwa kwa milango, watoto wadogo kuwekwa uvunguni kimazingara, nyumba kufagiliwa na  tukio kubwa la mke wa Mwalimu Rawlence John ambaye ni Mkuu wa shule Kanderema ‘B’ kujifungua Kokwa za Parachichi zenye chale na hirizi nyeusi.


    Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi Kayombo aliwataka wananchi wa Kijiji cha Bugoji kuachana na dhana potofu ya ushirikina badala yake wawe msaada kwa walimu hao ili waweze kutimiza majukumu yao kiufasaha na hatimaye kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.


    “Nimesikitika kusikia mambo ya kishirikina yanayoendelea kufanyika hapa, madaftari yanasahihishwa kimazingara, watoto wanasweka uvunguni, milango inafunguliwa kimazingara, wanafunzi wanaanguka hovyo madarasani ikaenda mbali zaidi mke wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kenderema ‘B’ Mwl. Rawlence John kajifungua Kokwa mbili za Parachichi zenye chale na hirizi nyeusi kwa Kweli sio jambo jema” alisema Kayombo.


    “Uchawi wa namna hiyo katika karne hii haupo, tunahitaji uchawi wa maendeleo, tunahitaji hospitali, shule na barabara nzuri, huo ndio uchawi wa maendeleo” alisema Kayombo.


    “Naagiza Mh. Diwani wa Kata ya Bugoji, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugoji, Wenyeviti wa kamati za shule za msingi Kanderema ‘A’ na Kanderema ‘B’ pamoja na wananchi muhakikishe swala hili ndani ya mwezi mmoja liwe limekwisha” alisema Kayombo.


    Baada ya kumaliza kikao hicho Mkurugenzi Kayombo aliongoza na waalimu pamoja na viongozi wa Kijiji kwenda kuona nyumba wanazoishi walimu waliopatwa na maswahiba hayo.

  • ← Prev
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • Next →

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI November 09, 2023
  • MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI (PSLE) KUANZA SEPTEMBA 10, 2025 NA KUMALIZIKA SEPTEMBA 11, 2025. September 07, 2025
  • TANGAZO LA HESABU ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 July 01, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2022 December 05, 2022
  • Angalia Yote

Habari za sasa

  • KIKAO CHA UTAMBULISHO CHA WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA CHAFANYIKA

    January 23, 2026
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KIKAZI KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI

    January 22, 2026
  • **ZIARA YA UFUATILIAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YAFANYIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA**

    January 20, 2026
  • TIMU YA WATAALAM WA MKOA NA HALMASHAURI WAANZA ZIARA YA UFUATILIAJI WA MIRADI - MUSOMA DC

    January 14, 2026
  • Angalia Yote

Video

KLABU YA LISHE YA SHULE YA MSINGI NYAMRANDIRIRA || MLO BORA
Video zaidi

Kurasa za karibu

Tovuti mashuhuri

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa