Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imefanya kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani ambapo agenda mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Wagombea wawili walijitokeza kugombea nafasi hiyo ambao ni Diwani wa Kata ya Bugoji Mh. Ibrahimundi M. Buruya kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Diwani wa Kata ya Bulinga Mh. Mambo J. Rebule kutoka (CHADEMA).
Wapiga kura katika Uchaguzi huo (Madiwani) walikuwa 28.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. John Kayombo alimtangaza Mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mh. Ibrahimundi M. Buruya kuwa mshindi wa Uchaguzi huo.
"Wagombea walikuwa wawili Mh. Ibrahimundi M. Buruya wa CCM na Mh. Mambo J. Rebule wa CHADEMA, wapiga kura walikuwa 28, kura zilizoharibika hakuna, kura halali 28" alisema Kayombo.
"Katika kura hizo mgombea wa CHADEMA Mh. Mambo J. Rebule amepata kura 5 na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Ibrahimundi M. Buruya amepata kura 23, kwa mamlaka niliyonayo napenda kumtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Ibrahimundi M. Buruya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Musoma kwa mwaka 2018/2019" alisema Kayombo.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa