Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, wamekamilisha zoezi la tathmini ya awali ya eneo lote pamoja na mapitio ya michoro ya awali inayoonesha mpangilio wa soko na majengo yatakayojengwa katika Mwalo wa Busekera, eneo linalotarajiwa kuanza ujenzi wa One Stop Center.
Baada ya kukamilika kwa tathmini hiyo, wataalamu hao walifanya kikao maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela Nitu Palela, ambaye alipokea rasmi taarifa ya awali ya mwenendo mzima wa mradi kwa niaba ya Menejimenti ya Halmashauri.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Palela, aliwashukuru kwa dhati wataalamu hao kwa ujio wao, ushirikiano waliouonesha, pamoja na hatua za awali walizochukua katika kutathmini eneo na michoro ya mradi huo muhimu, hatua ambazo zimeweka msingi mzuri wa utekelezaji wa ujenzi wa One Stop Center katika Mwalo wa Busekera.
Ilielezwa pia kuwa taarifa hiyo ni ripoti ya awali inayotoa mwelekeo wa jumla wa utekelezaji wa mradi, ikiwemo hatua zilizofikiwa, maandalizi yaliyokamilika, pamoja na mapendekezo ya kitaalamu kabla ya kuanza rasmi kwa hatua za ujenzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma itaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi, kwa kuzingatia taratibu, viwango na ratiba zilizopangwa, kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya sekta ya mifugo na uvuvi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa