Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma ikiongozana na Mkuu wa Wilaya Mhe. Juma Chikoka Leo Machi 11,2025 imetembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Kwa Mwaka 2020/2025.
Akikagua Ujenzi wa Ofisi za pembeni(Side Office) katika jengo la makao makuu ya Halmashauri, Mhe. Chikoka amesema, " Tangu nianze kazi yangu kama Mkuu wa Wilaya sikuwahi kuona majengo yakijengwa Kwa viwango na ubora wa juu kama hapa katika Halmashauri hii , Kila kitu kipo katika Halmashauri yetu ! Huu ni mtego kwa watumishi katika Halmashauri hii kwani Mhe. Rais anataka kuona matokeo bora ya utendaji kwa watumishi".
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. Msongela Palela amempongeza Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kwa kuiomba Serikali Kuu kutoa pesa kiasi Cha Tshs. 350,000,000 za kujenga Ofisi 16 za pembeni jengo la Makao makuu kwa ajili ya wataalamu mbalimbali .
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa