Kamati ya Mikopo ngazi ya Halmashauri imeanza mchakato wa kufanya tathmini ya maombi ya mikopo yaliyowasilishwa na vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2025. Jumla ya fedha zilizowasilishwa kwa ajili ya kuombwa mikopo ni Tsh 700,827,000/= ambazo zinatokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Maombi yaliyowasilishwa yanagawanyika kama ifuatavyo:
Katika zoezi hilo la tathmini, Kamati inalenga kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kilichoombwa kinaendana na miradi iliyowasilishwa na kuwa na uhalisia. Aidha, kamati inafanya uhakiki wa uhai wa vikundi, wanachama wake, uwezo wao wa kutekeleza miradi pamoja na kupima uelewa wao kuhusu shughuli wanazofanya na malengo ya mikopo wanayoomba.
Zoezi hilo ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa mikopo inayotolewa inalenga kuchochea uchumi wa vikundi husika, kuongeza kipato cha wanachama na kuleta maendeleo chanya katika jamii kupitia matumizi sahihi ya fedha za mikopo.
Halmashauri inaendelea kusimamia utekelezaji wa sera ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ili kuwezesha makundi maalum kiuchumi na kuwapatia fursa ya kupanua shughuli zao za uzalishaji.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa