Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira imefanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya kwa lengo la kupokea taarifa na kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanyika katika ngazi ya vijiji.
Katika ziara hiyo, Kamati ilitembelea Kijiji cha Busekera ambako ilipokea taarifa na kukagua shughuli zinazofanyika katika eneo la Mwaloni pamoja na stendi ya magari yaendayo Mikoani. Aidha, Kamati ilitembelea Kijiji cha Chirorwe kwa ajili ya kupokea taarifa na kukagua shughuli za uchimbaji zinazoendelea katika kijiji hicho. Ziara hiyo pia ilijumuisha Kijiji cha Sanya Bwai, ambapo Kamati ilipokea taarifa na kukagua ujenzi wa choo pamoja na shughuli nyingine zinazotekelezwa katika eneo la Mwaloni.
Ziara hiyo ilifanyika tarehe 22 Januari, 2026, ikiwa ni sehemu ya jukumu la Kamati la kufuatilia, kusimamia na kuhakikisha shughuli za kiuchumi, ujenzi na mazingira zinatekelezwa kwa mujibu wa mipango na taratibu zilizowekwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa