Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg.Msongela Palela katika ukumbi wa Makanya uliopo Kata ya Mugango Kiji cha Kwibara amefanya kikao na wakuu wa shule za sekondari na Msingi,Wenyeviti wa vijji na Vitongoji, Watumishi ngazi ya vijiji na Kata pamoja na viongozi ngazi ya Halmashauri kwa dhumuni la kuboresha utendaji katika vijji vyetu hasa utoaji wa elimu bora "Serikali zetu za vijji zimejipangaje katika zoezi la utoaji wa chakula shuleni?" Ameuliza Mkurugenzi Msongela ambapo Ndg. Richard Charles ambaye ni mwenyekiti wa Kiji cha Bulinga amesema sababu kubwa ya wazazi kutochangia chakula cha wanafunzi mashuleni ni matumizi mabaya ya vyakula hivyo kwani vinatumiwa na walimu badala ya wanafunzi na hivyo hawaoni umuhimu wa kuchangia chakula. Sambamba na hilo amesema kuwa ubora wa chakula kinachotolewa shuleni ni mdogo hivyo kupelekea chakula hicho kutoliwa na Watoto wao hivyo hawaoni haja ya kuchangia chakula ambacho Watoto wao hawakitumii
Ndg.Msongela amesisitiza jamii zetu kushiriki katika utoaji wa chakula shuleni kwani chakula ni hitaji la msingi na sio anasa na mtoto mwenye njaa hawezi kusoma. Tunapochangia chakula, tunachangia
afya,mahudhurio na mafanikio ya wanafunzi wetu. Ndg. Msongela ameahidi ubora na usalama wa chakula hicho. "Tunaandaa kinyago ambacho kwa kila kata itakayokuwa ya mwisho katika zoezi hili itakichukua na kukaa nacho kwa mwaka mzima ila kwa Kata itakayofanya vizuri nayo itazawadiwa". Amesisitiza Mkurugenzi
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa