Shule ya Msingi NYETASYO imepata elimu ya Kilimo cha umwagiliaji wa MATONE na kupata bahati ya kuwekewa na wadau wa kilimo mfumo wa UMWAGILIAJI wa MATONE katika BUSTANI ya Shule ya mbogamboga na matunda. Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Shule katika Kilimo Cha BUSTANI.
Aidha, Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyetasyo anatoa shukrani za dhati kwa wadau husika na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kupitia Divisheni ya afya chini ya Afisa Lishe Ndugu. Clement Bundi pamoja na Divisheni ya Elimu Awali na Msingi kwa kuwaunganisha na wadau husika.
PAMOJA TUNAWEZA!
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa