Maadhimisho ya SALIKI yanaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, ambapo wananchi wanaendelea kunufaika na huduma muhimu za afya pamoja na elimu ya masuala ya kijamii.
Huduma zinazotolewa katika maadhimisho hayo ni pamoja na utoaji wa matone ya Vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto, utoaji wa elimu kuhusu afya na lishe kwa watoto na mama wajawazito, elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, pamoja na elimu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira. Aidha, wananchi wanaendelea kupata huduma ya upimaji wa VVU kwa hiari.
Maadhimisho haya yanalenga kuimarisha afya ya mama na mtoto, kuongeza uelewa wa masuala ya afya na kuchangia ustawi wa jamii kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa