MAFUNZO YA MFUMO WA IMES YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA PAMOJA NA MAAFISA ELIMU KATA
Posted on: August 2nd, 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. Msongela Nitu Palela ameongea na Maafisa Elimu Kata, Watendaji wa Kata pamoja na vijiji Leo Agosti 1, 2024 katika Ukumbi wa Charles Magoma uliopo Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya akifungua Mafunzo ya Mfumo wa Tathmini na Ufuatiliaji (IMES) Kwa ngazi ya vituo vya kutolea huduma (i.e shule za Msingi ,shule za Sekondari, zahanati,vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya)
"Nawaomba mfuate utaratibu na Sheria katika utekelezaji wa majukumu yenu katika maeneo yenu, nami nawaahidi kuwalinda".Amesisitiza Ndg. Palela
Akiongea kuhusu kizazi hiki Cha Teknolojia, Ndg. Palela amewaasa Watendaji wa Kata, Vijiji pamoja na Maafisa Elimu Kata kujizoesha matumizi ya Teknolojia maana Serikali imehamia katika matumizi ya Teknolojia kwenye utekelezaji wa majukumu yake. Hii inaambatana na matumizi ya mifumo mbalimbali ya kielektroniki kama upimaji wa utendaji wa watumishi kazini(ess),mfumo wa manunuzi(nest),Tathmini na Ufuatiliaji (Imes) na mingine mingi hivyo Kila mmoja aendelee kutafuta uzoefu katika matumizi ya Teknolojia