Makarani waongozaji wa uchaguzi Jimbo la Musoma Vijijini, wamehimizwa kusimamia viapo vyao na kujiepusha kuwa chanzo cha malalamiko na vurugu wakati wote wa zoezi zima la upigaji kura siku ya Jumatano Oktoba 29, 2025.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu. Magange Hamis Mwita, ameyasema hayo leo Jumamosi, Oktoba 25, 2025, wakati wa shughuli ya ufunguzi wa mafunzo kwa makarani hao. Amesisitiza kusoma vyema katiba, sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo ya tume ilikuufanya uchaguzi kuwa huru na haki kama ilivyo dhamira na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

"Ni vyema mkajiepusha kuwa chanzo cha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kwa kushirikiana vyema na mawakala wa vyama vya siasa watakaokuwa kwenye vituo vyao kwa mujibu wa sheria," amesema Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Musoma Vijijini.
#KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura
#oktoba2025
#tumehuruyataifayauchaguzi
#uchaguzi2025
#UchaguziMkuu
#uchaguzi
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa