Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Evans Alfred Mtambi leo amefunga Kongamano la Wajasiriamali Mkoa wa Mara na kuwataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha na kurejesha mikopo kwa wakati, Mhe. Mtambi pia amewataka wajasiriamali wa Mkoa wa Mara kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili kuwachagua viongozi watakaowasaidia kutimiza ndoto zao za mafanikio
Mhe. Mtambi pia amezindua ofisi ya wafanyabiashsra ndogo ndogo Mkoa wa Mara zilizopo eneo la Majita Road, Manispaa ya Musoma na kuwataka wajasiriamali kutumia ofisi hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa Sambamba na Kongamano, wajasiriamali wa Mkoa wa Mara wamefanya matembezi ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa mafanikio waliyoyapata katika
kipindi cha uongozi wake.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa