Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Dkt. Khalifan Haule Leo Januari 22,2024 katika ukumbi wa Halmashauri amewataka Watendaji wa Vijiji kusimamia ulinzi na usalama katika vijiji vyao. Amewakumbusha kwamba wao ndio walinzi wa amani katika maeneo yao hivyo wanapaswa kuwajibika kwa kuhakikisha usalama wa Wananchi.
Dkt. Haule amemuagiza Mratibu wa Tassaf Wilaya Ndg. Separatus Mbanga kutembelea vijiji vyote 68 ili kutoa ufafanuzi kwa wanufaika walioondolewa kwenye Utaratibu wa malipo na kujibu kero zinazowakumba wanufaika wa mradi wa Tassaf.
"Kuna vifaa vilivyoletwa Kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yetu ambavyo havijatimia(Pungufu) hivyo nakuagiza uvifuatilie Ili tujue hitimisho lake. Mimi pia nitafatilia Kwa njia zangu mwenyewe" Dkt. Haule akimwagiza Mratibu wa Mradi wa Tassaf.
Dkt. Haule amesisitiza uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la awali ,Darasa la kwanza pamoja na waliochaguliwa kujiunga Sekondari wanatakiwa kwenda bila kikwazo chochote.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa