Leo kimefanyika kikao cha Wakuu wa Divisheni na Vitengo cha utambulisho kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mhe. Samweli Akello Maregesi.
Kikao hicho kililenga kumpa fursa Mwenyekiti kuwatambua Wakuu wa Divisheni na Vitengo mbalimbali pamoja na majukumu yao ndani ya Halmashauri, ili kuimarisha ushirikiano, uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Katika kikao hicho, Wakuu wa Divisheni na Vitengo walijitambulisha mmoja baada ya mwingine na kueleza maeneo wanayosimamia, huku Mwenyekiti akisisitiza umuhimu wa mshikamano, mawasiliano ya karibu na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na maslahi ya wananchi.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uongozi na usimamizi wa shughuli za maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa