Mwenyekiti wa Maafa Wilaya ya Musoma Mhe. Dkt. Khalifany Haule akiambatana na Kamati ya usalama Wilaya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya Ndg. Majidu Kalugendo Leo Februari 7, 2024 wamewatembelea wanakijiji wa Kijiji Cha Kabegi pamoja na Kamguruki kwa ajili ya kuwapa pole na kutoa msaada wa chakula (Mahindi na Maharage) vitakavyowasaidia katika kipindi hiki kigumu baada ya kukumbwa na Maafa yaliyoletwa na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha Usiku wa kuamkia Tarehe 5, Februari 2024.
Jumla ya Nyumba 17 zimeezuliwa paa na Nyumba 2 kubomoka katika Kijiji Cha Kabegi.Katika Kijiji Cha Kamguruki Nyumba 3 zimeezuliwa paa na Nyumba 1 kubomoka Kuta na kusababisha Kifo Cha mtoto wa Miezi 9 aitwae Wambura Dickson Wambura.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha kabegi Ndg. Charles Choto amemshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Khalifany Kwa kuwa bega Kwa bega na Wananchi wa Vijiji hivi kwani amekuwa nao tangu Tarehe 5 majanga haya yalipotokea Kwa ulinzi pamoja na huduma muhimu za kijamii Kwa waliofikwa na janga hili.
Pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha kamguruki Ndg. Alvin Wanzagi Amemshukuru pia Mhe. Mkuu wa Wilaya Kwa kuwagusa Wananchi katika kijiji chake kilichoathirika. "Serikali ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haijawahi kuwa nyuma katika kuwasaidia Wananchi wake" Amesisitiza Ndg.Alvin.
Diwani wa Kata ya Nyakatende Mhe. Gerald Mfungo Kasonyi Ameishukuru Serikali ya awamu hii Kwa kuwajali Wananchi wake na kuahidi kufanya kazi bega Kwa bega na Serikali Kwa juhudi zake za kusaidia wananchi . Mhe. Kasonyi ametoa mchango wake wa Sabuni Kwa familia zote zilizokumbwa na janga hili na kuahidi kuwa sambamba katika uimarishaji wa makazi ya wahanga wa Vijiji hivi.
Dkt. Haule amewashukuru Wenyeviti wa Vijiji hivi pamoja na wakazi wa Vijiji hivi Kwa kuonesha Moyo wa upendo wa kuwasaidia Wananchi waliopata majanga haya pia Kwa michango yao waliyochanga Tshs 200,000/= Kwa ajili ya kusaidia Kaya zilizoathirika. "Pia naishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Kwa michango yake kwenye Vijiji hivi Ili kuwasaidia waliokumbwa na janga hili " Dkt. Haule akishukuru .
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa