Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Mwakilishi wa Wafanyakazi Tanzania Mhe. Dkt. Alice Kaijage ametembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma pamoja na kufanya mazungumzo gikiwa ni pamoja na kero za Watumishi katika Halmashauri Leo Julai 16, 2024 katika Ukumbi wa Charles Magoma uliopo Suguti-Kwikonero.
Akiwasilisha baadhi ya Kero,Bi. Agnes Mshiu(Afisa Utumishi) amesema anaomba stahiki za watumishi wengine tofauti na kada ya ualimu ziweze kuzingatiwa kwani kundi hili huwa linasahaulika na mara nyingi fedha za malipo ya stahiki hizi kama uhamisho na likizo hutegemea mapato ya ndani hivyo kupelekea kutolipwa kwa wakati tofauti na kada ya ualimu ambao fungu lao huja moja kwa moja kutoka Serikali kuu.
Pia Bi. Agnes ameomba fedha za mikopo kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa kutoka Serikali Kuu kuongezwa kwani kiasi kinachokuja kwa sasa hakitoshelezi mahitaji ya watumishi wote kama ilivyokuwa imekusudiwa.
"Naishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kuwapandisha watumishi vyeo na nakuomba Mhe.Dkt Alice utufikishie salamu zetu za shukrani kwa Mhe. Rais wetu kwa kazi kubwa anayoifanya" Bi. Agnes akihitimisha.
Mhe. Dkt. Alice amewahakikishia watumishi kuwa mambo mengi ambayo ni kero kwao wameshayaongelea Bungeni na ataendelea kuyaongelea mpaka aone yametatuliwa hivyo waendee kuwa na Imani na Serikali yao inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na amewataka kumuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika awamu hii ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura .
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa