Siku ya Afya na Lishe ya kijiji cha Kusenyi, kata ya Suguti, imefanyika leo tarehe 3 Desemba 2025 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ya kata na vijiji. Viongozi hao ni pamoja na Mtendaji wa Kata ya Suguti, Afisa Maendeleo wa Kata, Mtendaji wa Kijiji cha Suguti, Mwenyekiti wa Kijiji, Tabibu wa Zahanati ya Suguti, wahudumu wa afya ngazi ya jamii pamoja na mwenyeji wa shughuli hiyo, Mtendaji wa Kijiji cha Kusenyi.
Katika maadhimisho hayo, wananchi walipata fursa ya kupata elimu na huduma muhimu za afya na lishe, lengo likiwa ni kuboresha ustawi wa jamii na kupunguza changamoto zinazotokana na utapiamlo na magonjwa yanayoweza kuzuilika. Huduma zilizotolewa ni pamoja na:
* Elimu ya afya na lishe kwa makundi yote ya jamii
* Matone ya Vitamin A kwa watoto
* Dawa za minyoo
* Upimaji wa hali ya lishe
* Elimu kuhusu usafi wa mazingira na umuhimu wa matumizi sahihi ya vyoo
* Uhamasishaji kuhusu utoaji na kuchangia chakula shuleni
Viongozi na wataalamu walioshiriki walisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kutumia huduma za afya, kuzingatia usafi, na kuhakikisha watoto wanapata lishe bora ili kujenga afya njema na maendeleo endelevu ya jamii.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa