Utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma ya matone ya Vitamini A umefanyika katika kipindi cha Septemba hadi Oktoba 2025. Utafiti huu umefuatia zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A kupitia Kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe kwa Mtoto iliyotekelezwa mwezi Juni 2025.
Lengo kuu la utafiti huo lilikuwa **kuthibitisha iwapo walengwa waliendelea kufikiwa na huduma za matone ya Vitamini A**, ikilinganishwa na kiwango cha uwafikishaji kilichoonekana wakati wa kampeni ya Juni 2025.
Matokeo ya Utafiti;
Ripoti imeonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imefanikiwa kuwafikia watoto kwa 83%, kiwango ambacho kiko juu ya kiwango kilichowekwa (kiwango cha viwango set standard ni 80%).
Matokeo haya yanaonesha kuwa Halmashauri imefanya vizuri zaidi ikilinganishwa na Halmashauri nyingine zilizoshiriki katika utafiti huu, ambazo ni:
* Musoma Municipal Council (MC)
* Butiama District Council (DC)
* Bunda District Council (DC)
Pongezi na Maelekezo.
Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg. Msongela Palela, ameipongeza timu ya watafiti pamoja na viongozi kutoka:
* Wizara ya Afya,
* Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI,
* Wadau wa Maendeleo (Helen Keller International),
kwa kutambua na kuthamini jitihada zinazofanyika katika utekelezaji wa afua za lishe ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Aidha, Mkurugenzi ameahidi kuendelea kusimamia na kutoa ushirikiano zaidi kwa timu ya wataalam wa afya na lishe ili kuhakikisha ufanisi wa juu zaidi unafikiwa katika utoaji wa huduma za lishe kwa watoto.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa