Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilayaya Musoma Ndg. Msongela Palela, amewataka Wananchi kutumia mikopo wanayokopa kufanya uwekezaji unaozalisha faida ilikuepuka kushindwa kufanya marejesho ya mikopo hiyo. Ndg. Palela alitoa rai hiyo wakati alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi za Serikali na Binafsi ambayo ipo Mkoani Mara kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali. "Kwenye Wilaya yetu kumekuwa na changamoto kwa Wananchi wetu kuchukua mikopo na hawaendi kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatazalisha faida ili watumie faida ile kufanya marejesho", alisema Ndg. Palela.
Aliongeza kuwa wananchi kukopa sio jambo baya lakini alitarajia mikopo hiyo iwasaidie lakini imekua tofauti kwasababu haiendi kutumiwa katika shughuli za uzalishaji hivyo wanashindwa kufanya marejesho Ndg. Palela alifafanua kuwa elimu ya fedha ni muhimu hivyo ni vyema Wizara ya Fedha ikahakikisha inawafikia Wananchi wote na elimu hiyo iwe endelevu kwakuwa inamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi endapo itaeleweka kwa wananchi wote.
Aidha, alizitaka Taasisi za Fedha zinazojihusisha na utoaji mikopo, kufuata utaratibu na Sheria zilizowekwa na Serikali ili mikopo wanayotoa kwa wananchi iwasaidie na isiwe chanzo cha kuongeza tatizo kwa kuweka riba kubwa zisizolipika kwa urahisi. "Naendelea kuwaomba watoa huduma za fedha kuwa waaminifu na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania za kuwalinda watoa huduma na wateja. Vilevile, aliwataka Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kujenga utaratibu wa kutumia Taasisi rasmi zinazotambuliwa na Serikali wanapohitaji mikopo, ilikuepuka udhalilishaji unaofanywa na Taasisi ambazo haziko rasmi na hazifuati utaratibu.
Ndg. Palela aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuendelea kuwachukulia hatua watoa huduma wanaofanyabiashara kinyume na utaratibu unavyoelekeza Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bw. Mbagira Kajanja, aliishukuru Serikali kwa kuwapatia elimu ya fedha ambapo alieleza kupitia elimu hiyo imewafumbua macho na kuelewa baadhi ya taratibu ikiwemo kuwa na haki ya kusoma mkataba kabla ya kuchukua mkopo.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa