Kupitia mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (Corporate Social Responsibility – CSR), Kampuni ya Polygold kwa kushirikiana na Ndugu Edwin Mchihyo wamefanikiwa kuchangia ujenzi wa Shule Shikizi ya Ekungu, hatua iliyoboresha mazingira ya elimu ya awali kwa watoto wa jamii ya Ekungu.
Katika kukagua utekelezaji wa mradi huo wa CSR, watu wa kampuni ya Polygold na Ndugu Edwin Mchihyo wakiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela Nitu Palela, pamoja na wataalam mbalimbali, walifanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo.
Katika ushirikiano huo:
Kampuni ya Polygold imejenga vyumba viwili vya madarasa na Ndugu Edwin Mchihyo amejenga vyumba viwili vya madarasa.
Ushirikiano huu wa CSR umeiwezesha Shule Shikizi ya Ekungu kufikia hatua muhimu ya utoaji wa elimu ya awali, huku ziara hiyo ikionesha dhima ya sekta binafsi na wadau wa maendeleo katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha elimu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa