MGENI RASMI ASHIRIKI UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NA LISHE KWA WATOTO WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI YA AFYA NA LISHE.
Katika uzinduzi wa Kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe kwa Mtoto uliofanyika leo 04 Desemba 2025 katika Kijiji cha Rukuba, Kata ya Etaro, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Msongela Nitu Palela, ameshiriki moja kwa moja katika ugawaji wa huduma muhimu za afya na lishe kwa watoto.
Akiwa kwenye eneo la tukio, Mkurugenzi Palela aliongoza zoezi la:
Kutoa matone ya Vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi 6–59, ambapo baadhi ya watoto alipokea na kuwapatia matone mwenyewe kama ishara ya uzinduzi wa rasmi wa kampeni hiyo.
* Kugawa dawa za minyoo kwa watoto wenye umri wa miezi 12–59, akisisitiza umuhimu wa kuwakinga watoto dhidi ya maambukizi ya minyoo kwa ajili ya afya bora na ukuaji mzuri.
* Kushiriki upimaji wa hali ya lishe kwa watoto wenye umri wa miezi 6–59, pamoja na ugawaji wa uji wa lishe kwa watoto waliobainika kuwa na changamoto za lishe, ili kuwapatia mlo wenye virutubisho muhimu.
Katika hotuba yake, Mkurugenzi Palela aliwahimiza wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi katika kampeni hii ambayo itaendelea hadi tarehe 31 Desemba 2025, akisema kuwa huduma hizi ni msingi muhimu wa kuhakikisha watoto wanakua wakiwa na afya njema na uwezo mzuri wa kujifunza wanapokomaa.
Afya bora ya mtoto ni msingi wa taifa lenye nguvu na maendeleo!
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa