Katibu Tawala wa Wilaya ya Musoma Ndg. Ally Said Mwendo Leo Mei 17, 2024 katika kikao Cha tathmini ya Mkataba wa Lishe Kwa robo ya tatu 2023/2024 amewataka Watendaji wa Kata kufatilia Wanafunzi wote ambao hawajaripoti katika Shule za sekondari walizopangiwa Kwa kuwachukulia hatua za kisheria Wazazi wanaokwamisha watoto wao kwenda shule.
Wakionge katika kikao hiki, Watendaji wa Kata wametoa Sababu mbalimbali za utoro wa wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na Wazazi kutengana, kufanya shughuli za uvuvi visiwani pamoja na Wazazi wa watoto kuhamia maeneo mengine Kwa shughuli za kiuchumi na hivyo kupelekea kutohudhuria shuleni." Taarifa za watoto wote ambao hawapo shuleni zimeshatolewa Polisi na wanaendelea kutafutwa". Watendaji wameripoti.
Akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa Mkataba wa Lishe Kwa robo ya tatu 2023/2024, Mratibu wa Lishe Wilaya Ndg. Bundi Clement amesema Kwa sasa zoezi la utoaji wa chakula kwenye shule zetu ni zaidi ya asilimia 90
"Sisi kama viongozi ni lazima tusimamie suala la usafi pamoja na Ujenzi wa vyoo katika maeneo yetu kwani Ugonjwa wa Kuharisha na Kutapika Bado upo. Naamini Kila mmoja atasimamia wajibu wake hasa katika Mazingira ya utoaji chakula mashuleni kwani yana mapungufu mengi hivyo yaboreshwe." Amesisitiza Ndg. Mwendo
"Suala la utoaji wa Fedha za Mkataba wa Lishe kutoka mapato ya ndani naamini Mkurugenzi atalisimamia maana sisi tumechoka kusemwa na kama hatafanya hivyo atajieleza mwenyewe maana katika tathmini ya Mkataba wa Lishe robo hii ya tatu inaonekana tuko kwenye alama nyekundu Kwa utoaji wa Fedha hizo Kwa asilimia 48". Amesiaitiza Ndg.Mwendo huku akifunga kikao hicho.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa