Ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa (Januari 20, 2026) katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imefanyika kwa lengo la kukagua kwa kina hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya ujenzi inayoendelea katika maeneo tofauti ya Halmashauri. Ziara hiyo imelenga kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu, ubora uliokusudiwa pamoja na muda uliopangwa kulingana na mikataba na mipango ya utekelezaji.
Katika ziara hiyo, timu ya wataalamu imefanya ukaguzi wa moja kwa moja katika maeneo ya ujenzi ili kujiridhisha na hatua zilizofikiwa, hali ya kazi zinazotekelezwa, pamoja na ubora wa vifaa vinavyotumika. Aidha, maelekezo mbalimbali ya kitaalamu yametolewa kwa mafundi na wakandarasi ili kuboresha utekelezaji wa kazi na kurekebisha mapungufu yaliyoonekana wakati wa ukaguzi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa